Kiungo cha kwanza ni Eurycoma Longifolia Extract. Watu wa asili wa Malaya wanakiita Tongkat Ali. Ni mti mrefu wa kijani wa kwenye vichaka unaopatikana kusini-mashariki mwa bara la Asia. Magamba na majani ya mti huu yametumika kwa muda mrefu kama dawa ya kuamsha tamaa ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake. Wanaume wa Malaysia wanadai kuwa chai iliyotengenezwa kwa mmea huu huboresha uwezo wa kufanya tendo la ndoa na urijali.
Katika miaka ya hivi karibuni, mmea huu umekuwa ukihitajika sana na kusababisha matumizi ya kiholela ya mmea huu wa asili. Kufuatia hali hiyo, mmea wa Eurycoma Longifolia umeorodheshwa katika mimea inayotakiwa kulindwa.
Utafiti umeonyesha kuwa B-carboline alkaloids na quassinoid-type glycosides ni viungo vikuu vinavyosababisha kupanda kwa viwango vya testosterone na kuongeza hamu ya kufanya mapenzi. Utafiti katika kliniki za binadamu umeonyesha kuwa Eurycoma ni dawa yenye nguvu ya kuamsha hamu ya mapenzi inayoboresha uwezo wa mwanamme wa kufanya mapenzi ikiwa ni pamoja na uume kuwa imara, uwezo wa kuzalisha, hamu ya kufanya tendo la ndoa, na viwango vya testosterone.
Lepidium Meyenii Walp Extract
Kiungo cha pili ni Lepidium Meyenii Walp Extract. Jina linalojulikana zaidi ni maca extract. Huu ni mmea unaoota kwenye milima ya Andes ya Peru, eneo lililo mita 4,000 juu ya usawa wa bahari. Eneo hili ni kame, lisilo na miti, lisilo rafiki kwa maisha ya binadamu, lenye jua kali, upepo mkali na mabadiliko makubwa ya halijoto. Hapa ndipo maca inapoota.
Simulizi zinasema kuwa wakati ufalme wa Incan ukiwa katika kilele chake, wapiganaji wa Incan walikula maca kabla ya kuingia vitani. Maca iliwapa wapiganaji hawa nguvu zaidi, uvumilivu zaidi na kuongeza kujiamini kwao. Lakini, baada tu ya kuuteka mji, wapiganaji hawa walizuiwa kabisa kutumia Maca, kwa sababu ingewafanya wawe na tamaa sana ya kufanya mapenzi. Zuio hili lilifanywa kuwanusuru wanawake wa mji uliotekwa.
Vilevile baada tu ya askari wa kihispania kuiteka Peru, wahispania na mifugo yao walianza kupata shida za kiafya na urijali kwenye ardhi ile kame ya milima ya Andes. Wenyeji waliwashauri wahispania hao kula Maca, wao na mifugo yao. Wahispania waliufuata ushauri wa wenyeji wao na muda si mrefu afya zao zilianza kuimarika.
Leo hii Maca inaelezewa kama ni chakula kikuu (superfood) kwa sababu ina uwingi wa virutubishi wa kutisha.
Jee, Maca ina nini? Ni chanzo kizuri cha protini, amino acids, fatty acids, vitamini, calcium, chromium, potassium, phosphorus, magnesium, sodium, iron, iodine, copper, manganese, zinc, selenium, uridine, sterol, glucosinolate, polysaccharide, flav-3ol, macaridine, macaene, macamide, maca alkaloids, beta-sitosterol, campesterol, stigmasterol, na glucosinolates. Baina ya virutubishi hivyo vyote, macamides na macaene ndivyo vitu viwili vinavyofanya kazi ya kibayolojia katika maca vinavyoongeza hamu ya mapenzi.
Herba Epimedii
Jina la kichina ni Yin Yang Huo. Jina hili linaelezea kuwa ni mmea wenye harufu nzuri unaongeza uwezo wa mbuzi kuzaliana. Jina hili lilitolewa na wachungajii waliogundua kuwa baada ya kula majani ya mmea huu, kondoo dume walisisimka na kuanza kuwapanda majike.
Watoa tiba wa kichina wa zamani waliutumia mmea huu kwa wanaume na waligundua kuwa majira ya joto, mmea huu uliboresha kidney yang, uliimarisha mfumo wa uzazi na kuongeza uwezo wa kufanya mapenzi kwa wanaume.
Utafiti ulionyesha kuwa Herba epimedii ina mchango kwenye utendaji wa mifumo ya C2+ influx na efflux. Vitu muhimu kiutendaji katika mmea huu ni flavonoids, alkaloids, na lignans. Na hasa, icariin, epimedin A, epimedin B, epimedin C na hyperin zinazoeleweka kuwa ni flavonoid glycosides zenye utendaji wa kibayolojia zilizo katika mmea huu na ambazo huongeza nguvu ya mwananme ya kufanya mapenzi.
Katika kliniki, Herba epimedii ilitumika kutibu ugumba. Pamoja na kuogeshwa mchanganyiko mwingine na kufanyiwa massage, utendaji wake ulifikia zaidi ya asilimia 90.
Withania Somnifera Extract
Mmea huu una majina mengi tofauti, kama Indian ginseng na water cherry. Mmea huu umetumika kwa ajili ya kutuliza msongo wa mawazo, kuongeza mkojo (diuretic), kupoza ubongo (sedative), antioxidant na kichocheo cha kufanya mapenzi katika nchi za India na China kwa maelfu ya miaka. Kemikali nyingi zimeonekana katika mmea huu. Vitu vya bayolojia vinavyofanya kazi zaidi ni withanolides, ambavyo ni triterpene lactones. Kuna withanolides tofauti zaidi ya 40, alkaloids 12 na sitoindosides kadhaa zimeonekana katika mmea huu.
Utafiti wa kwenye kliniki ulifanywa kwa kuwapa mmea huu wanaumw wagumba kwa miezi mitatu. Baada ya tiba hiyo damu zilichunguzwa. Matokeo yalionyesha uboreshwaji wa kikemikali wa damu zao. Pamoja na mambo mengine, homoni zao za uzazi ziliboreshwa.
Flos Caryophylli Extract
Jina linalojulikana sana ni clove (karafuu).
Jicho la ua (flower bud) la karafuu tangu enzi za kale limetumika kama dawa ya kuongeza hamu ya kufanya mapenzi ili kutibu matatizo ya kimapenzi ya wanaume. Utafiti kwa wanyama ulifanywa kwa kuwalisha panya mchanganyiko mzito na kufuatalia tabia yao ya kupandana. Ilibainika kuwa tabia fulani ziliboreshwa, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya marudio ya kupandana, muda unaopita kabla ya kurudia kupandana, usimamaji wa viungo vyao. Matokeo hayo yalionyesha kuwa karafuu ni mmea asilia wa kutibu matatizo ya uzazi.
Tiba ya asili ya kichina (TCM) inaamini kuwa utendaji wa karafuu unatokana na uwezo wake wa kuzipasha joto figo na kuuimarisha mkondo wa figo (kidney yang). Wanaume wanaoanza kupata maumivu na udhaifu wa kiuno na magoti wanakuwa wanaonyesha dalili za awali kabisa za kudhoofika kwa utendaji kazi wa figo na mfumo wa uzazi, kwa hiyo wanahitajika waanze kutumia kidney tonifying ili kuziamsha figo zao.
Herba Cistanches Extract
Jina la kichina la mmea huu ni Roucongrong. Ni mmea wenye thamani, ambao ni tiba baina ya matabibu wa kichina.
Mmea huu hupatikana sehemu kame au zenye ukame wa kiasi wa maeneo ya Eurasia na Afrika kaskazini, kama nchini China, Iran, India na Mongolia. Umetumika kwa karne nyingi katika tiba asili ya kichina kwa ajili ya kuongeza uwezo wa wanaume wa kuweza kuzalisha. Hadithi inasema kuwa Genghis Khan alikula mmea huu kila siku ili kuongeza uwezo wa uume wake kusimama na afya ya korodani.
Kemikali nyingi zenye uwezo wa kufanya kazi kibayolojia na kuongeza uwezo wa kuzalisha zimeonekana ndani ya mmea huu. Kemikali hizi ni phenylethaniod glycosides, iridoids, lignans, oligosaccharides, na polysaccharides.
Utafiti uliofanywa kwa wanyama ulionyesha kuwa panya waliopewa herba cistanches waliweza kuwa na uume unaosimama imara na mara nyingi zaidi kuliko wengine kwenye kundi lao. Vile vile panya waliopewa mmea huu walikuwa na viwango vikubwa zaidi vya homoni za uzazi.
Herba cistanches ina tabia za vasorelaxant-maana yake, inapunguza mkazo kwenye kuta za mishipa ya damu, na kuruhusu damu kupita kirahisi zaidi kwenda maeneo yanayohusika, pamoja na uume. Sababu kubwa ni kwamba herba cistanches inaongeza utengenezwaji wa nitric oxide ambayo inaweza kutanua ateri.